Monday 3 March 2025 - 17:35
Kupanua shughuli za shirika la habari katika lugha 11 / Hitaji la kuimarisha zana za vyombo vya habari vya ndani ili kukabiliana na udhibiti wa kimataifa

Leo, habari za Seminari (Hawza) zinachapishwa katika lugha 11, na Mwenyezi Mungu akipenda, ifikapo mwisho wa mwaka, tovuti za lugha hizi zote zitaamilishwa kikamilifu.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Hawza, Hojjatul-Islam wal-Muslimin Reza Rostami alipongeza kuwasili kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika mkutano wa vyombo vya habari na kuuona Mwezi huu kuwa ni fursa maalum ya kumtumikia Mwenyezi Mungu Mtukufu na kusema: Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa fursa ya kuufahamu Mwezi huu uliobarikiwa. Mwezi ambao masaa yake ni masaa bora na siku zake ni siku bora zaidi. Mwenyezi Mungu ametualika sote katika tafrija hii, na Mwenyezii Mungu akipenda (Insha Allah) atatujaalia kufanikiwa kuutumia (kufaidika na) Mwezi huu kikamilifu.

Akirejelea matembezi / msafara wa Arbaeen ya Husseini, aliuita kuwa ni mojawapo ya alama kuu za kimungu katika zama hizi na akaongeza: Kuadhimisha alama za kiungu ni mojawapo ya wajibu wetu. Mwenyezi Mungu anasema katika Qur'an:

"وَمَن یُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَی الْقُلُوبِ"

"Na wanaoziadhimisha alama za Mwenyezi Mungu, basi hilo ni katika Ucha - Mungu wa nyoyo."

Leo, tuko katika hali ambapo makampuni ya habari na vyombo vya habari vya kimataifa viko chini ya mrengo wa ukafiri, na vyombo vyetu vya habari vinakabiliwa na vikwazo vingi. Hata majukwaa ya ndani yanakabiliwa na changamoto katika uchapishaji wa maudhui za kidini.

Hojjat-ul-Islam wal-Muslimin Rostami alisema kwamba habari zinazohusiana na Arbaeen ya Hosseini zimedhibitiwa sana katika anga ya mtandaoni na akasema: Mwaka huu tulipata fursa ya kufanya mikutano maalum kuhusu udhibiti wa vyombo vya habari vya Arbaeen na tulichambua suala hili kutoka nyanja mbalimbali. Licha ya mapungufu yote, ni lazima kutumia zana zilizopo kwa njia iliyokuwa bora.

Mwishoni, Hojjatul-Islam Wal-Muslimin Rostami, akizungumzia shughuli za Shirika la Habari la Hawza, alisema: Shirika la Habari la Hawza limepanuka kutoka lugha nne katika Mwaka 2022 hadi lugha 11 katika mwaka wa 2024. Leo, habari za Seminari (Hawza) zinachapishwa katika lugha 11, na Mwenyezi Mungu akipenda, ifikapo mwisho wa mwaka, tovuti za lugha hizi zote zitaamilishwa kikamilifu.

Ikumbukwe kwamba Mkutano huu uliambatana na uwepo wa Vyombo vya Habari na Mubalighina wa Kimataifa, na mwisho, juhudi za Kituo cha Vyombo vya Habari vya Seminari (Hawza) zilipongezwa na kuthaminiwa.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha